JUMUIYA YA WAZAZI CCM IRAMBA WAPANDA MITI KATIKA KITUO CHA AFYA KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 47 YA CCM

 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Iramba, mkoani Singida, Michael Lemy (katika), akiwaongoza wanachama kwenda kupanda miti  katika kituo cha Afya, Kata ya Urughu, wilayani humo, ikiwa ni maadhimisho ya miaka 47 ya CCM. (Picha na Hemedi Munga)

MWANDISHI WETU 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Iramba, mkoani Singida, Michael Lemy, ameahidi kuendeleza kampeni ya upandaji wa miti.

Lemy amesema kampeni hiyo inatokana na upandaji  miti alioufanya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Januari 27, mwaka huu wakati akishiriki kupanda miti zaidi ya 4,000 kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Amesema huo ni mwendelezo wa kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa CCM, pia ni utaratibu wa maisha katika eneo lao la utawala.

Lemy amesema lazima kila mmoja ashiriki upandaji miti kwa lengo la kutunza mazingira na kupata hewa safi itokanayo na miti ya vivuli na matunda.

Aida Lemy amewataka wanachama wa CCM kuendelea kuhudhuria katika mikutano ya Chama  kusikiliza makubwa ambayo CCM imeisimamia serikali kufanya katika kila eneo kwa sekta zote.

"Ndugu zangu hakika ukomavu wa chama hichi unatokana na viongozi wake ngazi zote kushiriki katika shughuli za maendeleo, hivyo kinatoa imani kwa kila mtu," amesema.

Kwa upande wa Katibu wa jumuiya hiyo, Iddi Kijamba, amesema viongozi wa Chama ngazi ya kata kufanyia kazi maagizo yanayotolewa ngazi ya wilaya.

"Ndugu zangu  chama kitachukua hatua dhidi ya wale wanaodaiwa kuwa na tabia ya uzembe wa kuzembea maagizo na vikao, chama ni watu na tunaheshimiana kwa vikao," amesema.

Maadhimisho ya chama hicho yameendelea kushika kasi kwa kendelea kusaji wanachama kwa kadi za kielektroniki na kutoa maelekezo mbalimbali kuelekea kilele cha maadhimisho hayo, Februari 05, mwaka huu.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCCM Wilaya ya Iramba, mkoani Singida, Michael Lemy,  akipanda mti katika Kituo cha Afya, Kata ya Urughu, wilayani humo.(Picha na Hemedi Munga).


Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Iramba, mkoani Singida, Iddi Kijamba, akipanda mti katika Kituo cha Afya, Kata ya Urughu wilayani humo.