RAIS DK. SAMIA AZINDUA UGAWAJI VIZIMBA VYA KUFUGIA SAMAKI NA BOTI ZA KISASA KWA WAVUVI KANDA YA ZIWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa Wavuvi wa Kanda ya Ziwa katika fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock), Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024. Wengine katika picha ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emanuel Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makalla, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Riziki Shemdoe pamoja na viongozi wengine.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega kuhusu Boti za Kisasa na vizimba vya kufugia Samaki kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwakabidhi mfano wa funguo Wawakilishi wa vikundi vya Uvuvi kwa ajili ya ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati akielezea kuhusu Samaki wa aina mbalimbali wanaopatikana katika Ziwa Victoria mara baada ya uzinduzi wa boti za kisasa pamoja na vizimba vya kufugia Samaki Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekeza jambo kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati akielezea kuhusu Samaki wa aina mbalimbali wanaopatikana katika Ziwa Victoria mara baada ya uzinduzi wa Boti za kisasa pamoja na vizimba vya kufugia Samaki Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.