DK. TULIA AFUNGUA KIKAO CHA JUKWAA LA WABUNGE WANAWAKE WA IPU NCHINI USWIS



 Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, amefungua Kikao cha 37 cha Jukwaa la Wabunge Wanawake wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika kituo cha Mikutano cha Kimaita cha Geneva nchini Uswis,  Machi 24, 2024.

Kikao hicho kimejadili taarifa ya Maendeleo ya Wanawake ya Mwaka 2023 iliyoonesha ongezeko kufikia asilimia 26.9 ikiwa ni ongezeko la nukta 0.4  zaidi ya miezi 12 iliyopita. 

Hata hivyo taarifa hiyo imeonesha anguko kwa nafasi za juu za Uongozi kwa baadhi ya nchi zilizokuwa zinaongozwa na Wanawake. 

Aidha, masuala mbalimbali pia yalijadiliwa yakiwamo Shughuli za IPU zitakazochochea na kuongeza usawa wa kijinsia, Mchango wa shughuli za Mkutano wa 148 zilizotokana na mtazamo wa kijinsia, Mwanamke mjenzi wa amani katika kuendeleza amani endelevu na kuchagua Viongozi wa ofisi ya Wabunge Wanawake wa IPU.