SIDE: CHAGUENI VIONGOZI WANAOKUBALIKA NA WANANCHI


Diwani wa Kata ya Kivukoni, Sharik Choughule (kulia), akikabidhi kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Said Side, taarifa ya utekelezaji wa Ilani Chama 2023/2024 Kata hiyo, katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.


Na MWANDISHI WETU

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Said Side, amewakumbusha viongozi wa Chama kuchagua wagombea wanaokubalika na wananchi, kuelekea katika wa uchaguzi wa serikali za mitaa, unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Side amesema hayo, wakati wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM Kata Kivukoni, katika ukumbi wa Karemjee, Dar es Salaam, ambapo amesema wanapochagua mtu mchafu wanakiweka Chama katika hali ya kushindwa.

"Kiongozi ambaye siyo mtu watu hatufai, pia hashiriki mambo ya Chama na anakuwa mbali na wananchi kiongozi kama huyo hatufai kabisa, tutamuacha, pia sisi viongozi wa wilaya hatutaka majina ya wagombea waliochaguliwa na wananchi", amesema.

Pia Side amempongeza Diwani wa Kata hiyo, Sharik Choughule, kusimamia vizuri Ilani ya CCM katika hiyo na kuwataka viongozi na wananchi kumpa ushirikiano wakati wote wa uongozi wake.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata hiyo, Sharik Choughule, ataendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali wa Kata hiyo.

"Tunamshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kutupatia fedha za maendeleo katika kata yetu, na sisi viongozi tunaendelea kusimamia miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa, pia namshukuru Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu kwa kuhakikisha kata yetu inapata maendeleo", amesema.

Sharik amesema baadhi ya miradi iliyotekelezwa ni uwekaji wa taa za barabarani, katika mitaa ya mtaa wa Sea View (Ruhinda), Kivukoni (Sokoine), ukarabati wa vyumba vya madarasa 3 katika Shule ya Msingi Bunge na ujenzi wa barabara ya Kimara kiwango lami mtaa wa Sea View.

Pia Uwekaji wa taa za barabarani katika mtaa wa Ghana, Hamburg/barabara ya Garden, ukarabati wa Soko la Kimataifa la Samaki Feri, ujenzi wa choo cha umma Posta ya zamani na ukarabati wa vyoo vya ofisi ya Kata.

Miradi mingine ni kupendezesha mji kwa kujenga mzunguko Ocean Road na Askari Monument Posta, Boti ya doria katika Soko la Kimataifa la Samaki Feri na uwekaji wa paving katika njia za watembea kwa miguu kwa baadhi ya mitaa ya Kivukoni.