KATIBU WA UWT IRAMBA AWAITA WANACHAMA NA WANANCHI KUHUDHURIA MKUTANO KATIKA VIWANJA VYA OLD KIOMBOI
Na HEMEDI MUNGA, Iramba
KATIBU wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilayani Iramba mkoani Singida, Judith laizer amewaongoza baadhi ya wajumbe wa chama hicho kuhamasisha wananchi na wanachama kuhudhuria mkutano mkubwa wa Katibu wa UWT mkoa huo.
Judith ametoa wito huo leo akiwa katika barabara kuu ya mjini Kiomboi wilayani hapa, ambapo amesema mkutano huo utafanyika Juni 05, 2024 katika kiwanja cha Old kiomboi mjini hapa.
Aidha, Judith amewakaribisha wanawake wote wa wilaya hiyo kufika katika mkutano huo ambao Katibu wa UWT mkoa huo, Martha Kayaga anatarajia kueleza mafanikio lukuki ambayo wameyapata katika kipindi cha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Mbali na hayo, Judith ameweka wazi kuwa Martha atazungumzia ujasiriamali kwa Wajasariamali, hivyo wanawake wote wasikose kwa sababu Rais Dk. Samia ameruhusu mikopo hiyo kutolewa.
"Mikopo ya asilimia 10 ambayo Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameiachia fedha zije kuwanufaisha wananchi, niwaombe tuendee kumuunga mkono Rais wetu na kuumpa ushindi wa kishindo ifikapo 2025," amesisitiza.
Aidha, amewaomba wanawake kuendelea kujiunga katika vikundi mbalimbali kwa lengo la kupata mikopo.
Reviewed by Gude Media
on
June 04, 2024
Rating:

