IGUNGA - TABORA
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha amemuagiza Mkurugenzi wa Kampuni ya Sinda Builing Contractor, Fredrick Mloita anayejenga majengo manne katika hospitali ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora kuendelea kutekeleza taratibu na kanuni za usalama mahali palazi.
RC Chacha ametoa agizo hilo leo wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imewezeshwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika Hospitali ya wilaya hiyo.
Aidha, amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Selwa Abdalla Hamid kwa kuendelea kusimamia ipasavyo miradi yote ambayo inaonekana kuwa imara na yenye ubora kwa kuzingatia viwango stahiki.
Akitoa taarifa fupi mbele ya mkuu huyo wa mkoa, Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Melchades Magongo amesema mradi huo unagharimu sh milioni 900 ambapo kuna jengo la wagonjwa wa nje, jengo la mionzi, jengo la kuhifadhia maiti na jengo la wodi ya wanaume.