Na Mwandishi wetu
Madereva wa pikipiki (Bodaboda), wameshauriwa kuzingatia uendeshaji salama wa vyombo hivyo kuepuka ajali ambazo zinasababisha ongezeko la idadi ya watu wanaopasuliwa nyonga na magoti.
Hayo yamesemwa na Daktari Bingwa wa upasuali wa nyonga na magoti wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dk.Violet Lupondo alipozungumza hivi karibuni.
Ameeleza kuwa, ajali za bodaboda zitaongeza idadi ya upasuaji wa kubadilisha nyonga na magoti kwa vijana wa umri mdogo ambao wanapatiwa matibabu hayo kwasasa kutokana na mivunjiko mibaya ya nyonga na magoti.
Sababu zingine kwa vijana yanayoweza letea kubadilisha nyonga , yanatokana na magonjwa kama Rhematoid Athritis, haemophilia , sickle cell na avascular necrosis ( secondary degenerative disease). ambapo magonjwa hayo huanza katika umri mdogo
Dk.Violet alitaja sababu kubwa kwa sasa za ubadishaji wa nyonga na magoti ni uchakavu ambao unaambatana na umri mkubwa ( primary degeretive joint disease), hali inayotokea zaidi kwa wazee.
Aliieleza kuwa matatizo haya yapo zaidi kwa watu wazima wanawake na wanaume.
Dk.Violet aliongeza kuwa, kutambua chazo mapema (screening) na kupata tiba mapema, itapunguza ubadilishaji wa nyonga na magoti mapema.
Ukigundulika mapema kuna njia mbadala kama kurekebisha matege, na knocked knee, lakini pia kuna dawa za kupunguza kasi ya uchakavu hasa kwa magonjwa haya ya vijana niliyotaja hapo awali, kupunguza uzito na kufanya mazoezi inasaidia kuondokana changamoto za magoti na nyonga
Amefafanua kuwa, matatizo haya yakigundulika mapema na kupata tiba inapunguza kasi ya uchakavu . Lakini wanaendelea kuongeza jitihada za kutibu vijana hao wa boda boda wanaopata mivunjiko mibaya kutokana ajali.
Ameshauri kuongeza jitihada madhubuti za kudhibiti ajali za bodaboda hususani vijana Ili kuokoa maisha yao na hatari hiyo ya kufanyiwa upasuaji wa nyonga na magoti wakiwa na umri mdogo, kwani uwezekano wa kurudiwa uko juu, pia inahitaji vifaa vya marudio na vina gharama kubwa.
Daktari Bingwa wa upasuali wa nyonga na magoti wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dk.Violet Lupondo. |