Kigahe akabidhi bati 120 kuezeka jengo la CCM tawi la Nundwe

Na MWANDISHI WETU

MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, ambaye ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, amekabidhi bati 120 zenye thamani ya sh.milioni 5, kwa viongozi wa Chama wa Tawi la Nundwe, Kata ya Ihalimba jimboni humo kuezeka ofisi hiyo ya tawi la CCM.

Akizungumza alipokuwa akikabidhi bati hizo, Kigahe alisema alisema lengo la kukabidhi bati hizo ni kuhakikisha viongozi wa Chama wanatoa huduma katika ofisi nzuri kutokana na kazi kubwa wanayoifanya.

"Nimetoa bati hizi bora za kisasa na himara kuwezesha uezekaji wa jengo la Chama Tawi la Nundwe ikiwa ni utekezaji wa agizo la Mwenyekiti wa Chama Taifa, Rais Dk.Samia wa kutaka ofisi za Chama zikarabatiwe vizuri viongozi watoe huduma katika mazingira mazuri," amesema.

Amewataka viongozi wa Chama Tawi la Nundwe kuhakikisha wanatumia vizuri bati hizo kuezeka jengo hilo na likamilike kwa wakati litumike kutoa huduma bora kwa wananchi.