Makalla-Kazi tuliyonayo kwasasa ni kuhakikisha CCM inashinda uchaguzi wa serikali za mitaa
Na MWANDISHI WETU
KATIBU wa NEC ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amesema kazi kubwa waliyonayo kwasasa ni kuhakikisha Chama kinashinda Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Mwezi Novemba Mwaka huu.
Makalla ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, alipokuwa anafungua Shina la Wavuvi Mjimwema, Kata ya Mji Mwema Wilaya ya Kigamboni katika ziara yake wilaya hiyo, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
"Kazi kubwa tulinayo kwasasa ni kuhakikisha Chama kinashinda kwa kishindo katika Uchaguzi ulioko mbele yetu wa Serikali za Mitaa, hivyo tunafurahi kuona matawi na mashina yakifunguliwa," amesema.
Amewapongeza viongozi wa shina hilo, kwa ufunguzi huo kwani limefanyika muda muafaka kipindi cha kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Reviewed by Gude Media
on
August 27, 2024
Rating:


