Na SUPERIUS ERNEST
TUME ya Ushindani (FCC), imeahidi kuendelea kutekeleza wajukumu yake ya kulinda ushindani nchini kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya serikali kufanikisha malengo kusudiwa ya kutoa huduma kwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio, alipokuwa akitoa shukrani kwa Mkurugenzi wa Ofisi ya kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Firimin Msiangi baada ya semina ya mafunzo iliyofanyika katika ofisi za Ushindani.
"Tunakushukuru kwa semina hii nzuri inayotoa miongozo mbalimbali ya serikali inayotakiwa kutekelezwa katika Taasisi mbalimbali za Umma na uzingatiaji wa nyaraka za serikali na walaka wa mwaka 2000 wa kuzingatia taarifa sahihi na salama za serikali," amesema.
Mkurugenzi Urio ameeleza kuwa, FCC watahakikisha wanatekeleza yote waliyoagizwa na ofisi ya kumbukumbu kuhakikisha kuwa yanatekelezwa na watayafanyia kazi.
Amesema, kila mtumishi wa FCC atasimamia majukumu yake ya kutekeleza wajibu wake kwa umma bila kuathiri unyeti wa serikali.
"Maagizo uliyoyatoa yanalenga sana kwetu sisi viongozi wa umma, pia, yanagusa watumishi wa taasisi ambao tunashirikiana nao katika kutekeleza majukumu ya serikali, hivyo tutahakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake," amesema.
Vilevile, Mkurugenzi Urio, amemshukuru Mkurugenzi huyo kwa kazi kubwa ya kutoa semina na mafunzo hayo yenye tija kubwa katika utumishi wao kwa jamii.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ofisi ya Kumbukumbu na uhifadhi nyaraka za serikali , Firimin Msiangi amepongeza FCC, kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kutimiza majukumu ya serikali hukuakiahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuwajengea uwezo wa kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia.