MTUMBUIDA - HATUWEZI ISAHAU TANZANIA MSUMBIJI KUPATA UHURU

Na MWANDISHI WETU

BOLOZI wa Msumbiji NChini, Ricardo  Mtumbuida amewaongoza wananchi wa Taifa hilo waishio nchini kutembelea makaburi ya waasisi wa Taifa hilo  waliopigania uhuru, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 tangu Taifa hilo kupata uhuru, huku akimshukuru Tanzania kwa msaada mkubwa iliyoutoa wakati wa ukombozi.

Balozi Mtumbuida ameyasema hayo,jijini Dar es Salaam, jana alipotembelea makaburi ya mashujaa na wapigania uhuru wa Msumbiji yaliyopo hapa nchini ikiwemo la Samora Michel lililopo Kinondoni, ikiwa ni maadhimisho  miaka 60 tangu Taifa hilo kupata uhuru.

"Siku hii ni siku muhimu kwa Msumbiji tunapotimiza miaka 60 ya uhuru, tuna jivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na waasisi wetu na hata sasa chini ya Rais Filipe Nyusi, ambaye ameongoza vyema kutuweka pamoja na kuwepo mafanikio," ameyasema

Mtumbuida amefafanua kuwa, katika maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru hawawezi kuacha kukumbuka kazi kubwa iliyofanywa na Chama Cha Ukombozi (Frelimo) kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), chini ya Mwalimu Julius Nyerere katika kuhakikisha Msumbiji inapata uhuru.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanamsumbiji Nchini, Cosmito Miguel, amesema wamefurahi kukusanyika kwa maadhimisho hayo ikiwa ni siku muhimu kwa wananchi wa Msumbiji kukumbuka uhuru wao na mashujaa wa Taifa hilo.