Na MWANDISHI WETU
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, Thobias Nungu amemshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa fedha nyingi alizopeleka wilayani humo kutekeleza miradi mbalimbali ya iliyoahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi hivyo kazi yao ni kumtafutia kura za kishindo 2025.
Nungu, amesema Ilani ya Uchaguzi imetekelezwa kwa kishindo, kupitia fedha alizotupa Rais Dk.Samia ambaye ametoa mabilioni ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo, tutaendelea kumuunga mkono.
"Unapozumgumzia maendeleo ya Korogwe, huwezi kuacha kumtaja Rais Dk.Samia kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuleta mabilioni ya fedha ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kuondoa changamoto za kupata huduma kwa wananchi, hivyo deni letu ni kumtafutia kura za kishindo.Tunasema Rais Dk.Samia mitano tena," amesema.
Amesema wanao mradi wa maji kupitia miji 28, ambao umeanzia Mwanga utafika hadi Wilaya ya Korogwe kutatua kero za wananchi za Maji na kumtua mama ndoo kichwani.
Ameeleza, mradi huo unaotarajiwa kukamilika mwaka huu Desemba, huku akipongeza mradi wa chujio la maji uliogharimu sh.bilioni 1.5, za mradi ambapo walipokea sh.miliomi 900 zingine za mradi wa chujio la maji.