NDONDO CUP DODOMA 2024 YAZINDULIWA KWA KISHINDO


Mavunde atangaza zawadi nono za washindi

Na MWANDISHI WETU

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde  amezindua rasmi ya Ndondo Cup Dodoma 2024 ambayo yanaratibiwa na Clouds Media Group kwa ushirikiano na mbunge huyo.

Katika Mashindano hayo yanayoshirikisha Timu 32,m Bingwa wa Mashindano atapata Tsh 15,000,000 na Mshindi wa pili Tsh 7,000,000.

Mavunde amezishukuru Kampuni za GSM na ASAS kwa kuwa sehemu ya ufadhili wa mashindano hayo ambayo yamelenga kwa kiasi kikubwa katika kuibua na kuviendeleza vipaji vya vijana wanamichezo.

“Ukiacha burudani,katika mashindano haya tumejipanga kuibua vipaji na kuviendeleza kwa kuwa sisi kwetu michezo si burudani tu bali kwetu sisi michezo ni AJIRA”Alisema Mavunde

Akizungumza katika mahojiano leo,Mratibu wa Ndondo Cup Yahaya Mohamed “Mkazuzu” amesema mashindano ya mwaka huu ya Ndondo yanabeba ujumbe juu ya elimu ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na pia kwa kushirikiana na Watu wa Marekani elimu inatolewa juu ya masuala ya Afya na hasa kujikinga na maambukizi ya UKIMWI.