NINA WEMBE WA KUWAKATA KUCHA CHAFU WAPINZANI ARUSHA -MWENYEKITI CCM TANGA

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tanga ,Rajab Abdallah amesema ameandaa wembe mkali wa kuwakata kucha chafu makada wa Chadema Mkoa wa Arusha wakiongozwa na  Godbless Lema  kwa kampeni yao waliyoanzisha Arusha.

Mwenyekiti Rajab ameyasema hayo Mkoani Tanga katika mkutano wa hadhara uliofanyika Tanga Mjini kupitia ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani mkoani humo.

"Nilipochaguliwa hapa Tanga, niliwaambia kuwa nitatokomeza upinzani hapa, wengi hawakuamini nilichokuwa na kisema, lakini kwasasa mmejionea wenyewe.Sasa nakule Arusha ndiyo hicho kinachoenda kutokea Arusha," alieleza.

Mwenyekiti Rajab alieleza kuwa Chadema hawana hoja zote zimetekelezwa na Rais Dk.Samia, hivyo kazi wanayoifanya kwasasa ni kukejeli wananchi ikiwemo wasafirishaji wa pikipiki.

Alisema wapinzani kazi yao ni kutembelea magari ya kifahari na wanapomaliza mikutano yao majukwaaani ni kuwakamua fedha wananchi badala ya kuwasaidia.