Shule za kata zimezalisha wabunge na mawaziri zisibezwe - Mkt CCM Tanga

Na MWANDISHI WETU

Mwenyekiti  wa CCM Mkoa wa  Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rajab Abdallah amevitaka vyama vya upinzani, kuacha upotoshaji na kubeza shule za sekondari za kata kwani zimezalisha viongozi wengi wakiwemo Wabunge na Mawaziri.

Rajab ameyasema hayo, katika kata ya Kipumbwi,  alipokuwa akiwahutubia wananchi, katika ,ziara yake ya siku tatu.

"Wakija hapa wanasema shule za kata haziwasaidii  masikini zinazalisha wamachinja, jambo ambapo sio kweli ni upotoshaji mkubwa.Shule za kata ni mawazo ya mazuri ya serikali kuwa saidia watoto wa Tanzania kupata elimu ikiwa ni sehemu ya kuongeza wasomi", amesema.

Ametolea mfano umuhimu wa shule hizo, alisema zimesaidia kuzalisha viongozi wa serikali wa Mkoa wa Tanga, ikiwemo Waziri wa Maji, Mbunge wa Jimbo la Pangani, Jumaa Aweso, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma  'Mwana FA', Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Ummy Mwalimu, Mbunge wa Jimbo la Korogwe vijijini, Mnzava.