MWENYEKI WA CCM TANGA ASISITIZA AMANI MSINGI WA MAENDELEO NCHINI

Na MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tanga, Rajab Abdallah amewasisitiza wananchi wa Tanga, kulinda amani iliyopo nchini iliyoasisiwa na waasisi wa Taifa akiwepo, Mwalimu Julius Nyerere na viongozi wengine waliofuata akiwepo Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, huku akiwataka kuvipuuza vyama vya upjnzania ambavyo vinchocheo uvunjifu wa amani.


Pia, ametaka wananchi kupuuza utopotoshaji wa Chadema kusema kuwa shule za sekondari za kata hazina tija ya kuwaendeleza watoto wa maskini jambo ambalo sio kweli kwani zimesaidia kuzalisha viongozi wengi nchini.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM, almeasema hayoi, Mkoani humo, alipokuwa akihutubia wananchi wa Kata ya Kipumbwi Jimbo la Pangani, alipokuwa akihitimisha ziara yake ya siku tatu Katika majimbo ya Pangani na Tanga Mjini 

"Wanauliza eti tumepata mafanikio gani tangu kupata uhuru, tutawajibu mafanikio makubwa ya kuwepo kwa amani na utulivu nchini ikiwa ni matunda ya viongozi wetu waasisi wa Taifa, chini ya Mwalimu Nyerere ambaye alifanya kazi kubwa ya kuweka misingi imara ya amani ambayo imetufikisha hapa tulipo," amssema.