KANYASU - TUNAFURAHI KUONA WACHIMBAJI WADOGO WAKIAMINIWA, KUKOPESHWA NA BENKI

 


Na MWANDISHI WETU

MBUNGE wa Geita Mjini, Costantine Kanyasu amesema maonyesho ya madini ya Geita yamekuwa fursa kubwa kwa wananchi wa Mkoa huo hususan wachimbaji wadogo kupata mikopo kutoka Benki Kuu itakayo wanufaisha kukua kiuchumi.

Kanyasu ameyasema hayo Mkoani Geita, alipotembelea mabanda katika maonesho ya Saba ya Teknolojia ya Madini.

Amesema kuongezeka kwa waonyeshaji katika maonesho hayo kumesaidia kuongeza tija zaidi huku makambuni ya fedha kama Benki Kuu ikiwa kichocheo na msaada mkubwa kwa wachimbaji wadogo kwani itawasaidia kupata mtaji na kufanya uwekezaji wa kisasa usioharibu mazingira.

"Tumefurahi kwamba, benki nyingi zimeanza kuwaamini wachimbaji wadogo na muwakopesha hususan wale wenye maeneo ya Uchimbaji na elimu ya kutosha," amesema.

Ameongeza, jambo lingine ni kuanza kutumika kwa sheria mpya iliyopitishaa na Bunge, inayoitaka Benki Kuu kuwa  na akiba ya dhahabu ambapo wamefanikiwa kwa sehemu kubwa na sasa linatekelezwa jambo ambalo linaongeza thamani benki kuu na kukuza uchumi wa nchi.