MAGAMBO - NIKO TAYARI KUWAONGOZA VIJANA KATIKA FURSA ZA UWEKEZAJI MADINI

Na MWANDISHI WETU

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),Manjale Magambo amewataka vijana kuchangamkia fursa kubwa za madini zilizopo mkoani humo kujipatia maendeleo.

Mwenyekiti Magambo ameyasema hayo Geita Mjini katika maonesho ya Saba ya Teknolojia ya Madini, wakati wa kongamano la mkutano wa uwekezaji wa madini kwa vijana. 

"Geita tumebarikiwa utajiri mkubwa wa madini, asilimia 40 ya dhahabu hapa nchini inapatikana hapa Geita, hivyo tutumie fursa hii, tuwekeza na kupata mafanikio zaidi nchini," amesema.

Amesema vijana wa Geita wasipo weza kuchangamkia fursa za uwekezaji wa madini kipindi hiki cha Rais Dk.samia ambacho uwekezaji wa madini umerahisishwa itakuwa vigumu kufanya hivyo katika kipindi kingine.

Amesema yuko tayari kihakikisha kuwasaidia vijana kuhakikisha wanafanya uwekezaji wa madini, kwa kujiletea maendeleo ya kiuchumi.