MNEC WAMBURA -IWE MVUA AU JUA, TUTAMUUNGA MKONO RAIS DK. SAMIA

Na MWANDISHI WETU

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Chacha Wambura amewataka wananchi hususan vijana kumuunga mkono Rais Dk.samia kwa kazi kubwa na njema anayoifanya katika kuwaletea maendeleo wananchi hususan sekta ya madini, hivyo wampe kura za kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Mhandisi Wambura ameyasema hayo Mkoani Geita, katika Mkutano wa Vijana na  fursa za uwekezaji katika madini, yaliyohusisha vijana na viongozi mbalimbali wa uchimbaji madini.

Alisema Rais Dk.Samia amefanya kazi kubwa ikiwemo kufungua fursa za uwekezaji madini ndani ya  kipindi chake  hivyo wamuunge mkono, kwa kuwatengenezea uchumi vijana.

"Tumpambanie wakati wote na muda wote, iwe mvua, iwe jua wakati wote tumuunge mkono,iwe kwa kukimbia au kugalagala, kwani, efanya kazi kubwa naya mfano kwa vijana.