Kilave aendelea kunadi wagombea asisitiza ushindi wa kishindo kwa mitaa yote ya jimbo la Temeke

Na MWANDISHI WETU

Mbunge wa Temeke, Dorothy Kilave ameendelea kufanya kampeni na kunadi wagombea wa Serikali za Mitaa jimboni humo, huku akisisitiza ushindi wa kishindo.

Kilave ameyasema hayo wakati akinadi wagombea wa Kata ya Sandari, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni za kunadi wagombea wa serikali za mitaa Wilaya ya Temeke.

Kilave amesema sababu za wagombea hao kupata ushindi wa kishindo ziko wazi kutokana na utekelezaji mkubwa wa Ilani ya Uchaguzi uliofanywa na Mbunge huyo na fedha zilizotolewa na Rais Dk.Samia.

Amesisitiza wananchi kujiandaa kuwapigia kura wagombea wa CCM, Jumatano Novemba 27, mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais Dk.Samia kwa kazi kubwa aliyoifanya.