Na MWANDISHI WETU
MJUMBE wa Kamati Kuu CCM, pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajab Abdallah, amesema Chama tawala kitaibuka na ushindi wa kishindo dhidi ya wapinzani kwani hajajipamga vyakutoshaa.
Mwenyekiti Rajab ameyasema hayo alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa Kampeni kuwanadi wagombea wa serikali za mitaa Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga.
Amesema CCM imejinga ipasavyo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwani imeweka wagombea imara nchi nzima, tofauti na wapinzani ambao hawajajinga na wameweka wagombea wachache katika baadhi ya maeneo.
Rajab amesema wataendelea kufanya kampeni za kistaarabu kuwanadi wagombea wa CCM na kueleza kazi zinazofanywa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.