MWENYEKITI WA CCM MKOA WA DAR ES SALAAM, MTEMVU, KUPAMBANA NA VIONGOZI WANAOPOKEA NA KUTOA RUSHWA






 

Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abasi Mtemvu, hata wavuliwa wanaotoa rushwa wakati wa uchaguzi katika ngazi ya Wilaya na Kata.

Mtemvu alitoa kauli hiyo wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM Kata ya Kivukoni katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

Amesema ameshawaambia viongozi wenzake wa Chama Mkoa, kwamba akigundua mtu anamsaidia aliyetoa rushwa atapelekwa katika kamati ya maadili.

"Pale kwangu napiga vita rushwa na huku chini mpige vita rushwa, hatuwezi kuendelea kupata viongozi wanaotoa rushwa, ndiyo maana tunapata viongozi wabovu, mbunge au diwani hapatikani kwa wananchi", alisema.

Mtemvu amesema katika uongozi akigundua mtu aliyepita amepita kwa kutoa rushwa ataondolewa na mtu mzuri akiyeachwa atapitishwa.

Amesema kama mtu ana fedha ahudumie jimbo lake au kata yake lakini asitarajie kutoa fedha mkoani kupata uongozi, suala hilo katika uongozi wake halitatokea.

"Hatutaki mambo ya rushwa tukipata taarifa furani anatoa rushwa tutakushughulikia, kura mlizonipa miwalipe kura rushwa hiyo siyo heshima au niwalipe kuwaonea watu, sitokubali kukatwa mtu mwenye uwezo au mwanaCCM, kwani mimi ni muathirika wa kukatwa.", alisema.

Pia amewataka viongozi kutowafanyia fujo wabunge na madiwani wakati wa kipindi hichi watumize majukumu yao na badala yake wasubili hadi muda wa uchaguzi utakapofika.

Mtemvu amesema kipimo cha mbunge ni utendaji katika jimbo lake na diwani utendaji katika kata yake, na wasifikilie kutoa fedha mkoani.

Naye Mbunge wa Ilala, Naibu Spika Mussa Zungu, amesema lazima tumpambamie Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kusema mambo mazuri anayofanya kwa wananchi.

Zungu amesema uongozi siyo kupiga makofi na kwenda bungeni bali ni kujenga mahusiano kati yako na wale anaowaongoza.

Kwa upande wa Diwani wa Kata hiyo, Sharik Choughule, amesema amefanikiwa kutekeleza ilani ya CCM kwa kiwango kikubwa kwa sababu ya ushirikiano mzuri anaoupata kutoka kwa viongozi wenzake.

Amesema yeye ni jukumu lake kuhakikisha anamsaidia Rais Samia, katika kutekeleza makujumu yake kwa ngazi kata.