DIWANI HANANASIF NYAMWIJA APELEKA MAJI BURE KATIKA MTAA WA KISUTU NA HANANAF PAMOJA KUKARABATI OFISI YA SERIKALI YA MTAA


Diwani wa Kata ya Hananasif, Wilfred Nyamwija, amezindua mradi ya visima vya maji katika mtaa wa Kisutu na Hananasif pamoja kukarabati ofisi ya serikali ya mtaa wa Hananasif, Wilaya ya Kinondoni.

Nyamwija alisema wakati kampeni ya uchaguzi alihaidi kupeleka maji katika mitaa hiyo, hivyo ametekeleza ahadi hiyo kwa wananchi hao pamoja na kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Amesema kulikuwa na changamoto ya maji kutokana na kisima kilichokuwepo awali katika mtaa wa Kisutu hakikua kinafanyakazi kutokana na kuchakaa pia pampu yake iliibwa.

"Wakati napita katika kampeni zangu za kuomba kuchaguliwa kuwa diwani, wananchi walikuwa wanatamani kisima kile kifanyekazi kutokana na chanagamoto ya kukosa maji, pia kulikuwa na shida ya maji kutokana na mabadiliko ya tabia nchi", amesema.

Nyamwija amesema wananchi watachota maji bure katika visima vyote viwili, ili kuwapunguzia bajeti ya kununua maji na lengo lake ni kusaidia wananchi.

Amesema visima vyote vitakuwa vinasimamiwa na viongozi wa mitaa yote wamedhibiti tatizo la wizi wa pampu na kwamba wanannchi wamehamaisika kuvilinda pamaoja na yeye mwenyewe atakuwa akivufuatilia kwa ukaribu.

Pia kuhusu ukarabati wa ofisi ya serikali mtaa wa Hananasif, Nyamwija amesema alichua uamuzi wa kukarabati kutokana na jengo la ofisi hiyo kuharibika.

Nyamwija amesema ofisi hiyo ilikuwa imeharibika na ilimbidi aikarabati upya iwe bora na kisasa. 

Diwani wa Kata ya Hananasif, Wilfred Nyamwija, akizindua mradi wa kisima cha maji katika mtaa wa Kisutu, wilayani Kinondoni, alichojenga kwa gharama zake.