MAKAMU WA RAIS DK. MPANGO AMEWATAKA WATANZANIA KUONGEZA JITIHADA KATIKA KUIMARISHA ULINZI KWA WATOTO KUWAEPUSHA NA VITENDO VYA UKATILI







 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Philip Mpango ametoa wito kwa watanzania kuongeza jitihada katika kuimarisha ulinzi wa watoto ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili vinavyo wakumba hivisasa.

Makamu wa Rais amesema hayo mara baada ya kushiriki Ibadaya Misa Takatifu ya Sikukuu ya Krismasi katika Parokia ya Kristo mfalme iliopo Veyula mkoani Dodoma. Ametoa wito kwa watanzania kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu kwa matendo ya kikatili kwa Watoto na kuacha dhuluma dhidi yao. Aidha amewasihi waumini na watanzania kwa ujumla kutimiza mahitaji ya watoto katika kuwatunza ikiwemo kuhakikisha wanapata elimu.

Halikadhalika Makamu wa Rais ametoa wito kwa watanzania kutumia fursa ya uwepo wa mvua zilizoanza kunyeesha hapa nchini katika kuzalisha mazao pamoja na kupanda mitii likuhifadhi mazingira.

Amesema ni muhimu suala la upandaji miti kuanza katika ngazi ya familia kwa kupanda miti mitatu kila familia na hivyo kupendezesha nchi na kulinda mazingira.

Katika ibada hiyo, Makamu wa Rais ameambatana na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango na ibada imeongozwa na Paroko wa Parokia ya Kristo Mfalme iliyopo Veyula Dodoma Padre SaimonKatembo.