Diwani wa Kata ya Mabwepande, Kinondoni, Mhajilina Kassim 'Obama', akizungumza na wananchi wa kata hiyo kuhitimisha mgogoro uliodumu kwa miaka 20 baina yao na Shirika la Maedeleo ya Jiji la Dar es Salaam (DDC), leo. (Na Mpigapicha Wetu). |
Na Mwandishi Wetu
Hatimaye wananchi wa
Kata ya Mabwepande wameridhia Shirika la Maendeleo ya Jiji la Dar es Salam
(DDC), kupima maeneo yao na kuwekewa mawe maalumu hatua inayohitimisha kuhitimisha mgogoro uliodumu kwa miaka zaidi ya 20.
Jana
kimefanyika kikao kilichowakutanisha wananchi
hao uongozi wa DDC na Diwani wa Kata ya
Mabwepande, wilayani Kinondoni,
Mhajilina Kassim .
Diwani Obama, amewataka wananchi hao kuridhia hatua hiyo na
kuhitimisha mgogoro huo ambao amesema unakwamisha maendeleo yao.
“Kwa niaba
ya wananchi wa Mbwepande , ninamshukuru
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa
kuteua viongozi wasikivu hatimaye
tumehitimisha mgogoro huu katika kipindi cha uongozi wake.
Katibu Mkuu
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo, MKuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Amos Makalla, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe, Mbunge wa Jimbo la
Kawe Dk. Josephat Gwajima wame saidia kufikia hatua hii,”amesema.
Ameeleza
ataendelea kuwatetea wananchi wake kuhakikisha kila mmoja anapata haki yake
kwani hakuna mvamizi wa ardhi katika eneo hilo.
“Hapa hakuna
mwananchi mvamizi bali hawa ni wananchi
wanyonge waliotapeliwa na kuuziwa maeneo
na baadhi ya watu. Na natoa onyo wale wote wanaoingia katika kata hii kutapeli ardhi huu siyo wakati wao,” amesema Obama
Mkurugenzi
wa DDC, Paulo Mhache, alisema hakuna mwananchi katika eneo hilo ambaye
nyumba yake itavunjwa.
“Lengo letu
ni kurasimisha eneo hili la Mabwepande. Kuhakikisha linapimwa na kila mwananchi
apate hati itakayosaidia kutambulika rasmi,”amesema Mhache.
Amesema DDC
ndiyo mmiliki wa eneo hilo na ana hati halisi lakini ni shirika hilo ni
mali ya serikali hivyo haliwezi kuwaumiza wananchi hao hivyo kuwataka
kuwa watulivu.
“Tulikubaliana
gharama za upimaji ardhi kila mwananchi ziwe sh. 8500 lakini diwni wenu aliomba
tupunguze hadi sh. 6500 kwa mita moja ya
mraba,”alieleza.
Ameeleza kwa
kutambua hali za maisha fedha hiyo haitalipwa kwa mkupuo bali italipa kwanza
asilimia 10 na kisha itakuwa ikilipwa
kidogo kidogo.
Ameaasa wananchi kuamini ardhi ni maisha hivyo wasikubari kuchochewa, badala yake kila mtu aangalie tija kwa
manufaa yake na familia yake.
Wananchi wameshukuru kwa hatua iliyofikiwa na
kumpongeza Rais Dk. Samia, kuhitimisha
mgogoro huo waliodai kwa kipindi kirefu uliwafanya wajione wanyonge.
Amina
Abdallah, mkazi wa eneo la Mwendo kasi
katika kata hiyo, amemshukuru Rais Dk. Samia
na kushauri malipo ya upimaji kupunguzwa zaidi kwani wananchi wengi
katika eneo hilo ni wanyonge.
“Tunaomba
tupunguziwe gharama ya upimaji kwani
wengi hatuna kipato kikubwa,”amesema
Agosti 10 mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla aliingilia
kati mgogoro huo unaohusisha heka 6000
za DDC na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ambazo zilivamiwa
Makalla
alieleza eneo hilo lirasimishwe na
kupima viwanja na wananchi kununua viwanja hivyo.