MUHENGA AFURAHISHWA NA UTENDAJI WA RAIS SAMIA

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, kutoka Wilaya ya Kilombero na Mtendaji Kata ya Kiberege, Mkoa wa Morogoro, Acley Muhenga (kulia), akiwa katika mkutano mkuu wa Chama uliofanyika, hivi karibuni, mkoani Dodoma.

 

NA MWANDISHI WETU

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, kutoka Wilaya ya Kilombero na Mtendaji Kata ya Kiberege, Acley Muhenga, amesema amefurahishwa na utendaji kàzi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Muhenga amesema Rais Samia, anafanyakazi kwa watanzania hivyo na wao kama watendaji wa chini wanatakiwa kumuunga  mkono kwa kujituma zaidi.

Amesema kitendo cha watendaji wa chini kujituma maeneo yao ya kàzi sawa na kumuunga mkono Rais Samia.

Muhenga amesema Mtendaji wa kata kikubwa ni kusimamia maagizo yote yanayotolewa katika ngazi ya juu lakini kubwa kusimamia ukusanyaji wa mapato.

"Sisi ndiyo wenye jukumu la kumfanya mama akubalike na wananchi wa ngazi chini kwa kutekeleza maagizo yake kwa maslahi ya watanzania wote", amesema.

Pia Mhenga amewahia kuomba kuwa mgombea ubunge jimbo la Mlimba na kushika nafasi ya pili baada ya kutanguliwa na Mbunge wa sasa Godwin Kunambi na Rose Rwakatare ambao walifungana kura.