MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA ILALA, SIDE AOMBA MAJENGO YA SERIKALI YASIYOTUMIKA KATIKA KATA YA MINAZI MIREFU, WAPEWE YAKASAIDIE JAMII



Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Said Side (wa pili kushoto), akikagua eneo litakalojengwa Kituo cha Afya na mwekezaji katika Kata ya Minazi Mirefu, Dar es Salaam.


Diwani wa Kata ya Minazi Mirefu, Godlisten Malisa (kulia), akimpa maelezo Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ilala, Said Side (katikati), wakati wakikagua majengo ya SUDECO, ambayo hayatumiki wanayoomba kwa shughuli za kijamii.







Diwani wa Kata ya Minazi Mirefu, Godlisten Malisa, akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Said Sde, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Mtendaji Kata.

Ofisi ya Mtendaji Kata ya Minazi Mirefu, ambayo haijakamilika.

 

Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Said Side, ameiomba serikali kutoa majengo ya SUDECO na Mamlaka ya hali (TMA), kwa Kata ya Minazi Mirefu, yatumike kwa shughuli za kijamii.

Side alitoa wito huyo, juzi, Minazi Mirefu, Dar es Salaam, wakati akiwa katika ziara ya kukagua majengo hayo, eneo litakalojengwa kituo cha polisi na ujenzi wa Ofisi ya Mtendaji Kata.

Side alisema majengo hayo ya SUDECO yanamilikiwa na Wizara ya Kilimo na yale ya TMA, yakipatakana yatasaidia kuondoa changamoto ya Shule ya Msingi, Sekondari na kituo cha afya au Zahanati.

"CCM ni tunaungana na wananchi wa kata hii kuiomba serikali ibadili matumizi ya majengo hayo kuwapatia kata hiyo ambayo yapo ndani ya kata hiyo, yatumike katika kutoa huduma za kijamii kwa maana shule na kituo cha afya, kata hiyo haina  kituo cha afya", alisema.

 Naye Diwani wa kata hiyo, Godlisten Malisa, alisema wakipewa majengo hayo yatasaidia katika kuwahudumia wananchi katika sekta elimu na afya, ambayo imekuwa changamoto katika kata yake.

"Naomba Mwenyekiti tusaidie mimi Diwani nimekwenda zaidi ya mara kumi Dodoma kufuatilia jambo hili, hivyo tutashukuru sana kama tutafanikiwa kuyapata majengo hayo yanayomilikiwa na serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Mamlaka ya hali ya hewa, ambayo kwa sasa hayatumiki" alisema Malisa.

Alisema anaimani na ujio wa Mwenyekiti huyo na kwamba serikali inaweza kuyabadiloisha matumizi yake na kupelekwa kuwahudumia jamii.