RAIS SAMIA AHITIMISHA MATEMBEZI YA UMOJA WA VIJANA WA CCM, WAKATI WA KUADHIMISHA MIAKA 59 YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan, akizungumza na viongozi mbalimbali na Vijana wa Umoja wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), wakati akihitimisha matembezi ya vijana hao kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika Kijiji cha Paje, Mkoa wa Kusini Unguja.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan, akipokea Bendera kutoka kwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mara, Marry Daniel, ikiwa ni kuhitimisha matembezi ya UVCCM katika shamrashamra za kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika Kijiji cha Paje, Mkoa wa Kusini Unguja.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan, akipokea Matembezi ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), wakati wa shamrashamra za kuadhimisha Miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Kijiji cha Paje, Mkoa wa Kusini Unguja.



Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan, akikabidhi vyeti kwa Wadau waliowezesha kufanikisha matembezi ya Vijana wa Umoja wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), wakati wa kuadhimisha Miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Kijiji cha Paje, Mkoa wa Kusini Unguja.