NGUBIAGAI AOMBA USHIRIKIANO KILWA





 

NA MWANDISHI WETU MAALUMU, LINDI

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai, amewaomba watumishi kufanyakazi kwa ushirikiano na kujenga mshikamano.

Ngubiagai amesema hayo baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Tellac,  Makao Makuu ya mkoa huo.

Amesema ili kazi yake ya ukuu wa wilaya iwe nzuri, lazima nipewa ushirikiano na watumishi wa ngazi zote ndani ya Wilaya hiyo.

Amesema ukuu wa wilaya ni mamlaka ya kumsaidia Rais ndani ya katika Wilaya kwa kufahamu na kutatua matatizo ya wananchi wa wilaya hiyo, hivyo watumishi wa ngazi zote wanatakiwa kuwa kitu kimoja.

 "Nashukuru narudi kilwa kwa mara nyingine hivyo naomba ushirikiano kama ilivyokuwa zamani kabla ya kupangiwa majukumu mengine na  tukishirikiana kwa pamoja kila kitu kitawezekana", amesema.

 Aidha Ngubiagai amesema aliungana na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Zainabu Kawawa, kwa kuwataka wazazi wa wanafunzi waliochaguliwa kwenda kidato cha kwanza kuhakikisha wanakwenda shule.

Amewataka wazazi kutoficha au kuwaozesha watoto wote wenye umri wa kwenda shule.