KATIBU MKUU CHONGOLO: TUMEKUJA NA SULUHU YA CHANGAMOTO ZA WANANCHI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo,  akizungumza na wanachama wa CCM Shina Namba 18, Kata ya Itaragwe, Kitongoji cha Matale, Halmshauri ya Wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabib, alipowasili mkoani Morogoro, katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na uimara wa Chama, kuzungumza na wana-CCM na makundi mbalimbali ya wananchi.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Oganaizesheni, Issa Haji Gavu, akizungumza na wanachama wa CCM Shina namba 18, Kata ya Itaragwe, Kitongoji cha Matale, Halmshauri ya Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.


Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema, akizungumza na wanachama wa CCM Shina namba 18, Kata ya Itaragwe, Kitongoji cha Matale, Halmshauri ya Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema, akiwa na  vijana wa Hamasa Mkoa wa Morogoro, baada ya kumaliza mkutano wa  wanachama wa CCM Shina namba 18, Kata ya Itaragwe, Kitongoji cha Matale.


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, akitia saini kitabu cha wageni kwa Balozi wa Shina Namba 1, Kijiji Cha Kidebya, akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema  na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM,Organaizesheni, Issa Haji 'Gavu' na viongozi wa Chama mkoani Morogoro.

 

MOROGORO

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, amesema dhamira ya Chama ni kuendelea kutafuta suluhu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi katika maeneo yao, zikiwemo miundombinu, Elimu, Afya, Kilimo, Maji na Ardhi.

Chongolo ametoa kauli hiyo, mkoani Morogoro, wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya Gairo, alipokuwa akianza ziara ya kikazi ya siku tisa, mkoani humo.

Kuhusu migogoro ya Ardhi, Chongolo amesema anatambua Mkoa wa Morogoro una changamoto ya migogoro ya ardhi, ambayo inasababishwa na baadhi ya watu kutozingatia suala la mipaka ya maeneo na kuzusha migogoro isiyokuwa na tija kwa maendeleo yao.

"Kubwa kwenye mkoa huu ni Changamoto ya Migogoro ya Ardhi ambayo inatokana na Wakulima na Wafugaji ambayo huchochewa wakati mwingine na Watendaji wa Serikali, ambao Wanashindwa kutimiza wajibu wao" amesema.

Kuhusu Suala la Maji, Chongolo amesema anatambua wilaya hiyo ina changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wa eneo hilo, ambapo Serikali inaendelea na jitihada za kutatua tatizo la maji.

"Lengo la kuja hapa ni kuja kuangalia Changamoto za mkoa huu, tumekuja wakati huu ili kuangalia vyanzo vya maji, tunajua wengi wenu hapa mnatumia maji ya visima, mpango Uliopo ni kuangalia namna ya kutega maji kutoka milimani ili hatimaye kuondokana na Changamoto ya maji" ameeleza Chongolo.

Kwa upande wa Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema, amesema CCM itaendelea kuzunguuka nchi nzima kwa kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi na kuzipatia suluhu ya kudumu, kutumiza dhamira njema ya Mwenyekiti wa CCM na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Katibu mkuu wa CCM, Chongolo ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho na kuzungumza na Makundi mbalimbali.