WATUHUMIWA WANNE WAMEKAMATWA WAKIIBA MABOMBA YA MRADI WA MAJI KIGAMBONI

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, SACP. Muliro J. Muliro


Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewakamata watuhumiwa wanne wakiwa wanaiba mabomba ya mradi wa maji wa Kisarawe II kwenda Kigamboni, eneo la Kibugumo. 

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, SACP. Muliro Jumanne, amesema watuhumiwa hao wamekamatwa Aprili 8, 2023, Kibugumo, wilayani Kigamboni wakiwa na mabomba aina ya PVC inchi 6, na gari yenye namba za usajili T. 719 AGL aina ya Mitsubish Canter.

Muliro amesema  jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kumkamata dereva wa Canter, Emanuel Msofe, mkazi wa Keko Magurumbasi na wenzake watatu wakiwa wanajianda kusafirisha mabomba hayo.

Ameongeza kuwa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, inafanya mahojiano ya kina na watuhumiwa hao ili kubaini kabla ya kuwakamata, wameiba mara ngapi mabomba hayo na mambomba mangapi yameshaiba.