MAKALLA AZINDUA BARABARA YENYE UREFU WA KM 7.8 MBWENI

 Amshukuru Rais Dkt. Samia kwa kutoa Shilingi Bilioni 12 za Ujenzi wa Barabara hiyo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla, amezindua Barabara za Mkwajuni, Kata ya Mbweni, zenye urafu wa Kilometa 7.8 ambazo ujenzi wake umegharimu zaidi ya S. bilioni 12.

Akizindua barabara hiyo,  Makalla amemshukuru na kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuidhinisha fedha za ujenzi wa barabara hiyo ambayo imekamilika kwa asilimia 100 na kuifanya Kata ya Mbweni kuwa ya kisasa kama Masaki.

Makalla amesema mradi wa barabara umeenda sambamba na kuondoa mafuriko yaliyokuwa yakisumbua Wananchi wa Mbweni kwa kipindi cha muda mrefu.

Aidha Makalla ametoa wito kwa wananchi wa Mbweni kuhakikisha wanatunza na kulinda miundombinu ya barabara hiyo ikiwa ni kutotupa taka katika mitaro, kutoharibu taa za barabara na kila nyumba kupendezesha mbele ya majengo kwa kuweka bustani.

Pia Makalla amempongeza Mkandarasi kutoka Kampuni ya King's Builders kwa kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo na kukabidhi kwa wakati ikiwa katika ubora* mzuri kwa mujibu wa mkataba.