SHIRIKA LA NVeP na BARRICK WATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU MKOANI MARA

 Shirika la Nos Vies en Partage Foundation (NVeP) na  Kampuni ya Barrick, wametoa msaada wa dola za kimarekani 10,000, kwa kituo cha Kulea Watoto wenye Ulemavu cha St.Justin Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, mkoani Mara, kuimarisha huduma za malezi na kuwajengea watoto  uwezo wa kujitegemea katika jamii.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, mwishoni mwa wiki, katika kituo hicho, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko, alisema  huo ni  utaratibu shirika  kuelekeza misaada katika masuala yanayolenga kuleta tija na manufaa ya moja kwa moja katika jamii zenye uhitaji.

Lyambiko alisema NVeP inajikita kutafuta fedha za kusaidia makundi maalumu katika jamii wakiwemo  wanawake, watoto na mengine yenye uhitaji wa ukuaji wa kiuchumi na hadi sasa imeshasaidia mashirika 12 nchini Tanzania.

“Leo tunakabidhi msaada wa Dola 10,000 katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalumu cha St. Justin kupitia NVeP,  Kituo hiki ni sehemu muhimu ya jamii yetu, kimeonesha kuwathamini watoto hawa kwa jinsi walivyo bila kuwabagua kwa rangi, dini au kabila,” alisema.

Pia alisema fedha zilizotolewa na Shirika la Nos Vies en Partage (NVeP), lililoanzishwa na kufadhiliwa na Rais,  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, kusaidia makundi maalumu ya   Wanawake, watoto na makundi mengine yenye uhitaji yasiofaidika na ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Kituo hicho, Sista Juliana,  ameishukuru Kampuni ya Barrick na shirika hilo,  kwakua msaada huo utapunguza changamoto zikiwemo za kitengo cha jiko katika kituo hicho, kuimarisha huduma za malezi na kuwajengea watoto hao uwezo wa kujitegemea katika jamii.

Juliana alisema Kituo cha St. Justin kinalea watoto wenye ulemavu wa viungo, mtindio wa akili na  wasiosikia  kwa kuwapatia huduma maalumu na muhimu, zikiwemo za chakula, malazi, matibabu, elimu na mafunzo ya useremala na ushonaji.

Pia alisema kituo hicho kilianzishwa mwaka 2006 na kinaendeshwa na Shirika la Masista Moyo Safi wa Maria Afrika wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma. 

Juliana alisema sasa kituo kina wafanyakazi 25, kinahudumia watoto 110, ambapo 75 wanaishi kituoni na 35 wanaishi kwa wazazi na walezi wao  nje ya kituo.

Naye Ernest Mwita, akitoa shukrani  kwa niaba ya watoto wenzake wanaolelewa katika hicho, Ernest Mwita, ameishuku kampuninya Barrick, kwa kuwajili na  kujitoa kuwasaidia  waweze kuwa katika mazingira bora ya kuishi na kupata maarifa wakiwa katika kituo hicho na kwa jamii.