RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO MADOGO YA MIUNDO YA WIZARA NA UTEUZI


Kufuatia kutungwa kwa Sheria ya Mipango ya Taifa ya Mwaka 2023 pamoja na uamuzi wa kuhamishia masuala a uwekezaji Ofisi ya Rais, hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Miundo ya Wizara na kufanya uteuzi wa viongozi kama ifuatavyo:-

Ameunda Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji ambapo amemteua Profesa Kitila  Mkumbo kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji. Profesa Mkumbo ni mbunge wa jimbo la Ubungo.

Ameunda Wizara ya Fedha ambapo amemteua Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Fedha.

Kabla ya uteuzi huu Mhe. Dkt. Nchemba alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango

Ameunda Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo amemteua Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji kuwa Waziri wa wizara hiyo.

Kabla ya uteuzi huu Mhe. Dkt. Kijaji alikuwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara.

Amemteua Bw. Lawrence Mafuru kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Taifa.

Kabla ya uteuzi huu Bw. Mafuru alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango (Usimamizi wa Uchumi).

Amemteua Bw. Elijah Mwandumbya kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (Usimamizi wa Uchumi), Kabla ya uteuzi huu Bw. Mwandumbya alikuwa Kamishna, ldara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango.