MWANGAZA WATOA MSAADA KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU PUGU SEKONDARI

Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake cha Mwangaza, Gaudensia Mgendera, amewataka wanafunzi wa Shule ya Sekondari Pugu wenye mahitaji maalumu wasikate tamaa na badala yake wasome kwa bidii.

Gaudensia amesema hayo, wakati wa wakiadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kikundi hicho, Pugu, Dar es Salaam na kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Amesema wanatakiwa kujikubali kama walivyo pamoja na kumuomba Mungu, awasimamie ili watimize malengo yao.

"Kuwa mwenye ulemavu siyo mwisho wa maisha kwani tuna viongozi mbalimbali wa ngazi za juu wenye ulemavu, wamejikubali na wamesoma kwa bidii hadi wamefika hatua hiyo walionayo", amesema.

Pia amesema wao kinamama ni walezi na wako tayari kwa kikundi chao watakachokipata watatoa kusaidia wahitaji.

Gaudensia amesema lengo la kikundi hichi ni kusaidiana kusaidiana kiuchumi na kijamii na kujiletea maendeleo.

Amesema kila mwezi wanakutana kwa kutoa ada na michango mbalimbali ya kijamii, ndiyo maana 

katika kusheherekea miaka 10 ya kikundi hicho wameamua kupeleka mahitaji mbalimbali kuwasaidi vijana wa shule hiyo wenye mahitaji maalumu.

Naye Makamu Mkuu wa shule hiyo Utawala, Ndimangwa Nzota, amesema wamefurahiswa na ujio wa kikundi cha Wanawake Mwangaza, kufika shuleni hapo kutoa msaada kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Amesema wanafunzi hao wanamahitaji makubwa ambayo wazazi na walezi wao wanashindwa kugharamia, hivyo wameshukuru kwa kikundi hicho kwa kuungana nao kutoa msaada huo.

Pia Nzota amesema wamepokea fedha Sh. 300,000 kutoka katika kikundi hicho kwaajili ya matengenezo ya mashine ya kufulia katika shule hiyo, anaomba wakati mwingine wasaidie katika miundombinu ya usafiri kwa wanafunzi hao.