MNEC GUNGU ATOA VITABU VYA UONGOZI NA MAADILI


Na MWANDISHI WETU

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (MNEC) Taifa, Emmanuel Gungu Silanga, ametoa  vitabu vya uongozi na maadili ya Chama, Katiba na Kanuni katika Kata zote za Mkoa huo, kwa  biongozi ambao wanaotaka kuomba uongozi ndani ya Chama. 

Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa CCM, yaliyofanyika Kata ya Nyaluwande, Wilayani Busega, amesema Vitendea kazi hivyo kwa viongozi wa ngazi ya kata vitawasaidia kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa na kukisaidia Chama kutekeleza majukumu yake vizuri.

“Kama mtakumbuka vizuri mwaka jana tukiwa Maswa wakati tunasherekea sherehe kama hizi niliahidi kutoa vitabu hivi kwa Mkoa mzima, leo navikabidhi hapa tukiwa tunasherekea miaka 47 ya kuzaliwa CCM", amesema. 

“Vitendea kazi hivi ni nyenzo nzuri kwa viongozi wetu kutimiza majukumu yao vizuri. Hii pia itawasaidia hata wale ambao wanataka kuwania nafasi za uongozi ndani ya Chama kujua kazi zao,”amesema.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohamed Seif,  amempongeza Gungu kwa kutoa vitabu hivyo ni msaada mkubwa kwa Chama, vitasaidia kuwajenga viongozi na kutambua  majukumu yao.

“Naomba nikupongeze sana MNEC Gungu, umefanya jambo kubwa sana vitabu hivi vitawasaidia viongozi wetu kuwaimarisha na kuwajenga vizuri kutekeleza majukumu yao naomba nichukue nafasi hii kukupongeza sana,”amesema.

Pia katika maadhimisho hayo MNEC ametoa mifuko ya saruji 30 ya ujenzi wa Ofisi ya Kata ya CCM Nyaluwande na kutekeleza ahadi yake  nyingine ya kutoa mifuko ya saruji 100 ya ujenzi ya Zahanati ya Kata ya Shigala, wilayani Busega.