ZAWADI 'MAGIFTI DABODABI' ZAMIMINIKA

Msemaji wa Shindano la Kampeni ya ‘Magifti Dabodabo’, Haji Manara, akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni tano mshindi, Monalisa Kasota baada kuibuka kidedea jijini Dar es Salaam jana.(Na Mpigapicha Wetu). 


MWANDISHI WETU

Zawadi zimezidi kutolewa kwa washindi wa Shindano la Kampeni ya ‘Magifti Dabodabo’ linazoendelea nchi nzima.

Katika droo iliyofanyika jana Dar es Salaam, washindi mbalimbali wamepatikana na kukabidhiwa zawadi zao.

Baadhi ya washindi waliopatikana na kupatiwa zawadi zao jana ni Monalisa Kasota, Hemed Swai (sh. milioni tano kila mmoja), Eliva Lazaro sh. milioni moja na Ismail Rashid aliyeshinda vifaa vya nyumbani.

Wakizungumza baada ya kupewa zawadi zao jijini Dar es Salaam jana, washindi hao walisema wamefurahia kuibuka kidedea na kwamba wataendelea kutumia miamala mbalimbali kuhakikisha wanashinda zawadi zaidi.

Eliva alisema zawadi ya sh. milioni moja alizozipata zitamsaidia kuendeleza biashara zake.

Amesema anawashauri wadau mbau mbalimbali kuendelea kutumia miamala kuhakikisha wanashinda zawadi zaidi.

“Nimefurahia kuibuka mshindi wa sh. milioni moja, hivyo ninaamini nitaendelea kutumia miamala mbalimbali kuhakikisha ninashinda zawadi zaidi,” alisema Eliva.

Monalisa aliyeshinda sh. milioni tano, alisema fedha hizo anatarajia kutatua changamoto mbalimbali zinazomkabili katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka.

“Nitaendelea kutumia miamala mbalimbali kuhakikisha ninashinda zawadi kubwa zaidi, fedha nilizozipata zitanisaidia kutatua changamoto mbalimbali za mwanzo wa mwaka,” amesema.  

Akizungumza wakati wa kuwakabidhi zawadi kwa washindi, Msemaji wa Kampeni ya ‘Magifti Dabodabo’ Haji Manara alisema shindano hilo linaendelea nchi nzima.

Amesema katika shindano hilo ambalo lilizinduliwa mwishoni mwa mwaka jana na litafanyika kwa siku 80, wamekuwa wakigawa zawadi mbalimbali kwa washindi.

Amezitaja zawadi ambazo zimekuwa zikitolewa kila wiki ni vifaa vya nyumbani, safari za Dubai, Zanzibar, fedha taslim hadi sh. milioni 10 na magari mawili mapya.

Amesisitiza kuwa kampeni hiyo inalenga kuwazawadia washindi zawadi za ‘Magifti Dabodabo’ wakiwa na wapendwa wao.

“Shindano la kampeni hii bado linaendelea ambapo tumekuwa tukitoa zawadi kwa washindi na watu wao wa karibu", amesema. 

“Washindi wamekuwa wakipatikana kwa kufanya miamala mbalimbali, hivyo tunawaomba wadau waendelee kufanya miamala kuhakikisha wanaibuka kidedea kwani zawadi bado zipo nyingi,” amesema.