DUWASA YAFANYA UKAGUZI WA MIUNDOMBINU YA MAJITAKA

 DODOMA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imeendelea na zoezi la ukaguzi wa miundombinu ya majitaka katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma ili kuiweka katika hali ya usalama.

DUWASA imebaini kuzidiwa na miundombinu ya majitaka eneo la Makole kutokana na baadhi ya wananchi kutokuzingatia matumizi sahihi ya miundombinu hiyo kwa kutupa taka ngumu katika chemba za majitaka na hivyo kusababisha kuziba kwa miundombinu ya majitaka.

Meneja wa Majitaka na Usafi wa Mazingira DUWASA, Mhandisi Daniel Mgunda, amesema zoezi hilo ni endelevu ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi.

Naye Rahel Muhando, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma DUWASA, amewataka wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya miundombinu ya majitaka kwa usalama wa afya.