Na MWANDISHI WETU, Dar es Salaam
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Qur'an ni chachu ya maadili mema kwa taifa kuwa na jamii bora yenye kumwelekea Mwenyezi Mungu
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo Dar es Salaam, katika kilele cha tuzo za Kimataifa za Qur'an Tukufu, zilizoandiwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'an Tanzania.
Amesema ustawi wa jamii uko ndani ya kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu, hivyo ni muhimu kwa jamii kuyafahamu maelekezo yake nakuyaishi na kufanikiwa hapa duniani na akhera.
Amesema kazi kubwa katika kujenga ustawi wa jamii ni kuimarisha maadili bora hasa kwa vijana.
"Hili linahitaji mikakarti imara kwa kuhakikisha hawaporomoki. Naipongeza jumuiya ta Kuhifadhisha Qur'an Tanzania mmekuwa mfano mwema kwa kuwa na shule zinazo saidia kulea na hatimaye kutoa wataalamu mbalimbali," amesema.
Mwinyi amesema hatua hiyo inasadia kuzalisha viongozi wazuri na raia wema katika taifa.
Amesema tayari wapo mamia ya vijana wa kitanzania waliohifadhi Qur'an na kuhitimu shahada za juu katika elimu ya dunia hivyo kuwataka wadau kuwasaidia vijana hao.
"Nachukua fursa hii kuwaomba wadau wengine kuziunga mkono juhudi hizi kwa kuwasaidia vijana walioandaliwa na kuhifadhi Qur'an huku wakiwa na fani mbalimbali", amesema.
Mwinyi amesema tuzo hizo ni chachu kwa washindi kuendelea kumtumikia Mwenyezi Mungu na kwa wengine kushiriki.
Rais Dk. Mwinyi amesema ataendeleza nyayo za Rais mstaafu Hayati Ali Hassan Mwinyi, katika kuielea na kuisimamia Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'an Tanzania.
Rais Mstaafu Hayati Mwinyi, alikuwa ni mlezi wa taasisi hiyo kwa zaidi ya miala 32 hadi alipofariki mapema mwaka huu.
Kwa upande wa Waziri Mkuu Kassim, Majaliwa, amepongeza taasisi zote za kuhifadhisha Qur'an hapa nchi kwa kuwa na mtiririko bora wa kupata washiriki kuanzia ngazi za chini kitaifa, Afrika na Kimataifa.
Amesema ni muhimu kuhakikisha wanapatikana watoto kuanzia umri wa miala 10 waliohifadhi Qur'an kama ilivyo kwa mataifa mengine yaliyotuma washiriki wenye umri huo.
Naye Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dk. Aboubakar Zubeir, amesema mashindano ya kuhifadhi Qur'an yameiitangaza Tanzania duniani.
Amesema Tanzania imekuwa ikopokwa sifa kwa kuandaa mashindano makubwa na kutoa vijana nyota wanao wika duniani kwa kuhifadhi kitabu kitufu cha Qur'an.
Mufti Zubeir ameitaka jamii kuwalea vijana hao na kuwafuatilia ili waendelee kuwa kielelezo cha maadili bora katika jamii.
Aidha alitoa malekezo kuwepo kwa somo la kuhifadhisha Qur'an katika madrasa na shule zinazofundisha malezi ya kiislamu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'an Tanzania, Sheikh Kapolo, amesema katika hali ya kusikitisha wakati wa kutafuta washiriki baadhi ya mikoa ilishindwa kutoa mshiriki hata mmoja kijana aliyehifadhi Qur'an na hata kukosa kabisa mshiriki wa miaka chini ya 12 ambaye angeiwakilisha Tanzania katika madhindano hayo.
Sheikh Kapolo aliwataka waislam kushiriki kilamilifu kusaidia kuwandaa watoto kuhifadhi Qur'an ikiwemp kuwawezesha walimu wa madrasa ambao wanafanya kazi kwa kujitolea.