Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, amemtembelea kumjulia hali mmoja wa Makatibu Wakuu Wastaafu wa CCM, Mzee Yusuf Makamba, Jumatatu, Aprili 1, 2024, nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Akimpongeza kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo na kumtakia heri kwenye majukumu hayo mapya.
Pia Mzee Makamba amemzawadia Balozi Dk. Nchimbi, sare ya Chama Cha Mapinduzi, ikiwa ni ishara ya kifaa cha kazi, ambapo alipokea pongezi hizo na kumshukuru kwa zawadi hiyo.