Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Igunga, Selwa Hamid. |
IGUNGA - TABORA
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Selwa Hamid kwa kushirikiana na Meneja wa Kanda ya Tabora wa Bohari ya Dawa (MSD), Rashid Omar wameahidi utayari wa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.
Viongozi hao wametoa ahadi hiyo, leo wakati wa kikao kazi kati ya Timu ya Usimamizi wa huduma za afya wilaya (CHMT) na Bohari ya Dawa ya kanda hiyo inayohusisha mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi katika hospitali ya wilaya hiyo mjini hapa.
Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi huyo, Selwa amesema wanaweza kufikia lengo hilo ikiwa wataendelea kudumisha utayari ambao wanaamini utawawezesha kufikia mafanikio.
Pia, amewataka wiongozi na watendaji hao kuendelea kujitathimini na kufanya kazi kwa kuzingatia ubora na viwango stahiki.