Na MWANDISHI WETU
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tanga, Rajabu Abdulrahman ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, amekabidhi sh.milioni 30 kwa madereva wa magari aina ya Costa na Daladala 600 kuwalipia ada ya mafunzo ya leseni ya udereva.
Akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo, jijini Tanga, Mwenyekiti Abdulrahman alisema kuwa lengo la kutoa fedha hizo ni kuwasaidia vijana kupata vyeti vitakavyo wawezesha kuuisha leseni katika kazi yao udereva kuwa na umahiri katika kazi yao ya kuwasafirisha abiria.
"Chama Cha Mapinduzi kinathamini vijana, ndiyo maana linaendelea kuwatengenezea ajira sawa Ilani ya CCM inavyoagiza, hivyo ndiyo maana tumeona tukabidhi kiasi hiki cha fedha kuwasaidia wajiendeleze katika kazi yao ya udereva wa usafirishaji abiria, hivyo kuepuka na kupunguza ajari na vifo
"Pia, nawapongeza viongozi wote wa CCM na serikali Tanga wakiongozwa na Mkuuu wa Mkoa, katika kuhakikisha ushirikiano wa kufanikisha jambo hili, ambapo kwa pamoja tunaendelea kumuunga mkono Rais Dk Samia kwa kazi njema anayoifanya," alisema.