Katambi - Tunatekeleza miradi yote tuliyoahidi kupitia Ilani ya Uchaguzi

Na MWANDISHI WETU

MBUNGE wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, ajira na wenye ulemavu), amesema wanaendelea kutekeleza miradi yote waliyoahidi katika Ilani ya Uchaguzi, kuwapatia wananchi huduma bora na kutatua kero zao.

Katambi ameyasema wakati akipokea Mwenge wa Uhuru, jimboni humo, ambapo Alieleza kuwa  miradi iliyokaguliwa na mwenge huo, ni mradi wa maji safi na salama  wa Kijiji cha Bugayambelele, uliopo Manispaa ya Shinyanga.

Amewapongeza watendaji wa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) Shinyanga, kwa kuongeza mtandao wa maji kwa kilomita 8.041, ambapo ilijenga kilomita 1.5 na SHUWASA ikajenga kilomita 6.459, hivyo kusaidia wananchi wengi kupata maji safi.

amewahakikishia wananchi wa jimbo hilo utekelezwaji wa miradi yote iliyoahidiwa katika ilani ya Uchaguzi,

Katambi amesema kutokana na machungu aliyonayo kwa wananchi wa Shinyanga, amekuwa akitafuta fedha kutekeleza miradi mingi ya maendeleo, amefanikiwa kutoa fedha za jimbo sh.milioni 61.6, ambazo zitatumika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kila Kata.

“Ahadi ambazo niliwahidi wananchi kipindi cha uchanguzi nyingi nimetekeleza na nina mshukuru Rais Dk. Samia kwa kuniunga mkono na leo kero nyingi zimetatuliwa ikiwamo miundombinu ya barabara  iliyokuwa korofi na madaraja,” alisema Katambi.

Amemshukuru Rais Dk.Samia kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya barabara, afya, maji na kuboresha huduma za wananchi wa Jimbo hilo hususan suala la nishati safi ambapo wananchi waligeiwa mitungi mbalimbali.