LATRA yawataka wamiliki wa kampuni za mabasi kuwapatia mafunzo wahudumu wa mabasi yao kabla mfumo wa usajili haujafungwa

 

MAMLAKA  ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imewaataka wamiliki wa makampuni ya mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani, kuhakiksha wahudumu wa usafiri huo wanapata mafunzo ya utoaji huduma na kupewa vyeti na kujisajiri katika mfumo wa Mamlaka hiyo kabla ya kufungwa kwa usajili huo Desemba Mwaka huu.

Hayo yamesemwa jana, jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Salum Pazzy, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwendelezo wa mafunzo na usajili kwa watoa huduma hao.

"Kwa mujibu wa sheria kifungu cha tano (1) E' Mamlaka ina jukumu la kusajili wahudumu wa magari ya kibiashara na sheria zinawataka kusajiliwa na LATRA, baada ya kupata cheti cha mafunzo katika vyuo husika," alisema.

Amewataka wamiliki wa makampuni ya mabasi hayo, kuhakikisha wahudumu wanasajiliwa hadi kufika  desemba 31, mwaka huu, kwani ikifika Januari wahudumu ambao watakuwa hawajapata mafunzo na kusajiliwa katika mfumo wa LATRA hawataruhusiwa kutoa huduma.6

Pazzy ametaja faida za kusajili wahudumu ni kurasmisha fani kwa utoaji bora wa huduma, kuongeza uwajibikaji, kuongeza umoja na mshikamano ambapo wahudumu wasajiliwe na kufahamika, kwani wameshapata mafunzo kupitia vyuo hivyo ikiwemo Chuo Cha Biashara (CBE) na Chuo Cha Taifa  (NIT).

Pia, amesema katika kujenga hali ya Ushindani  LATRA, imeeandaa tuzo maalumu kwa watoa huduma masafa marefu, ambapo wamesha tangaza utoaji wa tuzo hizo, waendelee kujitokeza ambapo zimegawanywa katika makundi mbalimbali washindi watatangazwa kilele cha wiki ya nenda kwa usalama barabara Septemba Mosi mwaka huu.