MFILINGE ASISITIZA UMOJA UWT PWANI

Na MWANDISHI WETU

KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Pwani, Kitte Mfilinge amesisistiza umoja kwa Umoja wa Wanawake (UWT) Pwani kwani ndiyo nguzo kubwa ya Chama katika ushindi na kufanikisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.

Pia, amemshukuru Rais Dk.Samia kwa kas yake ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi huku akiahidi kuendelea kumuunga mkono kwa kusimamia vyema utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkoa huo.

Katibu Mfilinge ameyasema hayo mkoani humo, alipokuwa wakizungumza na Baraza la  Kawaida la UWT, huku akisisitiza umoja na mshikamano.

"Sisi tumekuja kuhakikisha tunawaunganisha na sio kuwatemganisha, kwani umoja ni msingi wa Chama katika kutekeleza majukumu yake ya kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama, " amesema.

Amesema wao kama viongozi watahakikisha UWT Pwani inakuwa moja na inafanya kazi kwa ushirikiano, kuhakikisha wanatimiza dhamira ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa UWT Pwani, Zainab Vullu alimpongeza Katibu Mfilinge kwa kuaminiwa na kuchaguliwa na Chama kuongoza Mkoa huo na kumuahidi ushirikiano wa kutosha.