Wananchi tufanye utalii wa ndani-Sharik


Diwani wa Kata ya Kivukoni, Sharik Choughule, amewaomba wananchi kufanya utalii wa ndani, ikiwemo kupanda Mlima Kilimanjaro.

Sharik amesema katika kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kukuza sekta ya utalii, amepanda Mlima Kilimanjaro, ambayo ilikuwa ndoto yake.

"Utalii siyo kwa wageni tu, hata sisi Wananchi tunapaswa kufanya utalii katika maeneo mbalimbali kuona vivutio vilivyopo, pia tushawishi wageni waje kwa wingi kutembelea maeneo ya utalii nchini", amesema.