Mwenyekiti wa CCM Tanga akabidhi sh.milioni 1.5 kununua mashine ya kuoshea magari na pikipiki

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tanga, Rajab Abdallah, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, amekabidhi sh.milioni 1.5 za kununua mashine ya kuoshea magari na pikipiki za vijana wa mabanda.

Akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo, alisema lengo la kukabidhiwa fedha hizo ni kuwasaidia vijana wanaotafuta kipato kwa njia halali.

"Nifuraha yangu kuona vijana wakiendelea kujishughulisha kupitia kipato halali.Nitaendelea kuwaunga mkono wakati wote nitakapoweza, vijana endeleeni kupambana katika njia sahihi na za haki," alisema.

Wakipokea fedha hizo, vijana hao wa Mkoa wa Tanga walimshukuru Mwenyekiti Abdallah kwa fedha hizo za kununulia mashine ambayo itasaidia kusafisha vyombo vyao vya usafiri kuzifanya vidumu zaidi.