Mwenyekiti wa CCM Tanga asisitiza uzalendo, ujasiri wa Lowasa na Sokoine

Na MWANDISHI WETU

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rajab Abdallah ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga ametembelea makaburi ya viongozi wastaafu wa serikali na Chama katika mkoa wa Arusha, huku akitaka jamii kuendelea kuyaenzi maisha ya viongozi hao kwa kuwa wazalendo, wachapakazi na wenye ujasiri katika maamuzi yenye maslai kwa Taifa.

Makaburi yaviongogozi yaliyotembelewa na Mwenyekiti Abdallah ni ya Hayati Edward Sokoine na Edward Lowassa, ambao walikuwa Mawaziri Wakuu wastaafu wa Tanzania, ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mkoa huo wa Arusha.