TUTASHINDA UCHAGUZI KWA KISHINDO-MKT CCM TANGA

Na MWANDISHI WETU

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tanga, Rajab Abdallah amesema kuwa wamejipanga vyema kuhakikisha wanashinda kwa kishindo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka huu, ikiwa ni ishara ya ushindi wa Uchaguzi Mkuu wa Mwakani.

Mwenyekiti Rajabu ameyasema hayo wakati akimkaribisha Malezi wa Mkoa huo, Hemed Suleiman Abdallah ambaye ni Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, alipofanya ziara Mkoa huo.

Mwenyekiti Abdallah amesema wamejipanga vizuri watafanya vizuri katika Uchaguzi wa serikali za Mitaa ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ambao utakuwa mwepesi kwao.

"Mwaka huu nilazima tufanye vizuri katika Uchaguzi wa serikali za mitaa ikiwa ni ishara ya ushindi wa Uchaguzi Mkuu, kwani Uchaguzi wa mwaka huu ni kama kombe la FA ambalo tushachukua na mwakani tunaenda kuchukua Ligi Kuu", amesema 

Amewahakikisha wanachama wa CCM Tanga kuwa watahakikisha wanachangua wawakilishi wazuri watakao kubalika kwa wananchi na sio wale wanao sababisha migogoro kwa wananchi kama ambavyo ameshuhudia kwa baadhi viongozi katika ziara yake.