BALOZI MULAMULA ASHIRIKI MKUTANO WA EURASIAN WOMEN NCHINI URUSI


Balozi Liberata Mulamula ambaye ni Mbunge wakuteuliwa, ameshiriki mkutano wa Jukwaa la Wanawake Duniani ambao  umefunguliwa rasmi leo Mjini St. Petersburg na Rais  wa Urus Vladmin Putin wa Urusi.

Balozi Mulamula ameshiriki Jukwaa hilo la nne tangu kuzinduliwa 2016, ambalo linajulikana kama Eurasian Women Forum, akiwakilisha Bunge la Tanzania, pia akishiriki mkutano huo kama mwalikwa kutoa uzoefu wake kama mwanadiplomasia mbobevu hususan mchango wa wanawake katika kuchochea amani na usalama ulimwenguni kupitia diplomasia.

Mkutano huo, umekuwa na washiriki wapatao 3,000 kutoka nchi 125, wakiwemo viongozi wanawake mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais wa Uganda, Mawaziri, Spika wa Mabunge mbali mbali duniani, Wabunge, Wanaharakati, Vijana, Wanasayansi na Wanazuoni mashuhuri.

Katika Mkutano huo Rais wa Mabunge Duniani, Spika  Dk.Tulia Ackson ambaye ni Spika wa Bunge la Tanzania, amehutubia mkutano kwa njia ya Video.